JIFUNZE NAMNA YA KUFANIKIWA KIMASOMO KUTOKA KWA ROSALIA! MWANAFUNZI WA NNE KITAIFA 2019

This is a Trial Version of Social Share & Locker Pro plugin. Please add your purchase code into Licence section to enable the Full Social Share & Locker Pro Version.

Leo tuna simulizi nzuri na ya kusisimua, ya mdada mrembo na msomi, Rosalia  ambaye alifanikiwa kuwa mwanafunzi wa nne kitaifa katika matokeo ya kidato cha nne 2019! Ungana nasi katika kujifunza kutoka kwenye simulizi yake ya mafanikio!

1.Tuelezee kwa ufupi, wewe ni nani?

Kwa majina naitwa Rosalia Asheri Mwidege, ni mtoto wa pili kuzaliwa kwa wazazi wangu. Kwa sasa nina umri wa miaka kumi na nane (18). Nimeishi Mbeya tangu kuzaliwa kwangu ilhali mimi ni Mkinga. Mama yangu ni mbena na Baba yangu ni mkinga. Nimesoma katika shule ya msingi Mkapa iliyopo jijini Mbeya kuanzia 2008 mpaka 2015 ambapo nilihitimu na kujiunga na shule ya Wasichana na St. Francis (St. Francis Girls’ Secondary School)  iliyoko Mbeya mjini kuanzia 2016 mpaka 2019. Nilihitimu kidato cha nne kwa kiwango cha juu kiasi cha kushika nafasi ya nne kitaifa , ya pili kwa wasichana, ya kwanza katika somo la Fizikia na nafasi ya tatu katika somo la Jiografia. Kwa sasa ninasoma United World Colleges East Africa,International School of Moshi,   kama wengi wanavyoifahamu  iliyoko Arusha.

2.Tuelezee ilikuaje kwako na ulimudu vipi kuhama kutoka katika Shule ya serikali kwenda kwenye shule ya Kingereza.

Kwa kweli, kwenda katika shule ya serikali ya mchepuo wa Kiingereza ilikuwa ni bahati kubwa katika maisha yangu ingawa sikwenda katika shule bora lakini nilijitahidi kufanya vizuri kwa msaada wa MUNGU ambapo nilifaulu vizuri sana shule ya msingi jambo lililonipa imani kuwa ninaweza kuwa bora hata nitakapokwenda sekondari cha msingi ni sala, juhudi na kazi. Hakika, haikuniwia vigumu kujiongeza ili kuendana na ushindani wa shule ya St. Francis ambapo ubora ndiyo chachu iliyonisukuma kujitoa mhanga na kufanya vizuri kimasomo.

3.Mbinu gani za kimasomo ulizitumia, kufanikisha ufaulu wako wa kidato Cha nne.

Ufaulu wangu wa kidato cha nne ulitokana na kumtegemea MUNGU na kumuamini kuwa Yeye ndiye mwezeshaji na hivyo ataniwezesha pia. Pamoja na hayo, kusoma kwa makundi kulisaidia sana katika kuboresha ufaulu wangu kwani siku zote mtu hawi bora akiwa peke yake, lazima kuna vitu anavitegemea kutoka kwa wanafunzi wenzake. Pale ambapo sikuelewa nilijishusha na kuwa mnyenyekevu tayari kwa kujifunza kutoka kwao. Rafiki, walimu na wazazi  wangu nao hawakubaki nyuma muda wote walinitia moyo kuwa ninaweza. Jambo lingine, ni kwamba vile vitu nilivyovielewa kwa undani zaidi nilitumia fursa hiyo kuwafundisha wenzangu jambo lililonipa umahiri katika mada na masomo husika.

4.Nini ndoto na kusudi lako kimaisha

Kimaisha nina ndoto za kuwa mjasiriamali hasa katika sekta ya kilimo na

ufugaji, mwanauchumi na mhadhiri ili kuisaidia na kuikomboa jamii na nchi yangu ambayo imekuwa ikivutwa nyuma na umaskini.

5.Kipi kinachokupa hamasa maishani ya kusoma kwa bidii

 Kila ninapokumbuka namna wazazi wangu wanapambana ili kunisaidia katika elimu yangu, ninapata nguvu na uchungu wa kusoma kwa bidii. Kwani wao walitokea katika familia duni  lakini bado waliweza kupambana na kupiga hatua kubwa kutoka kwa wazazi wao. Hivyo kama wazazi wangu kutoka familia duni walipambana na wakaweza basi hata mimi nikipambana nitaweza kupiga hatua kubwa zaidi katika kuikomboa familia, jamii na nchi yangu kwani waliohamisha milima walianza na mawe madogo madogo.

6.Unadhani elimu ya Tanzania, ifanyiwe maboresho ili itimize kusudi au lengo halisi la elimu.

Elimu ya Tanzania inatakiwa ijumuishe mafunzo ya ujuzi wa maisha na karama mbalimbali kama vile sanaa, michezo na fani mbalimbali ili kuwaandaa wananchi kujiajiri na sio kuajiriwa.

7.Una ushauri gani kwa wazazi, Wana mchango gani katika mafanikio ya mwanafunzi yoyote?

Wazazi wana mchango mkubwa katika mafanikio ya mwanafunzi kwani wazazi wangu waliniombea, walinitia moyo na pia walinipa mahitaji yote yaliyohitajika ili kuhakikisha nasoma kwa amani na furaha jambo ambalo limechangia kwa kiasi kikubwa katika ufaulu wangu.

8.Mwisho, Toa maneno matatu ambayo n ushauri kwa wanafunzi wengine.

SALA, KAZI NA JUHUDI!

Related Articles

SIMULIZI YA MAFANIKIO YA HOPE – MWANAFUNZI BORA KITAIFA 2018
ONE ON ONE:JINSI NILIVYOFAULU MITIHANI KUPITIA MAKTABA
NECTA Yatangaza Matokeo Darasa la Saba, Tazama Hapa
JIFUNZE NAMNA YA KUFANIKIWA KIMASOMO KUTOKA KWA ROSALIA! MWANAFUNZI WA NNE KITAIFA 2019

Recently Viewed

More articles will be added latter

3 responses on "JIFUNZE NAMNA YA KUFANIKIWA KIMASOMO KUTOKA KWA ROSALIA! MWANAFUNZI WA NNE KITAIFA 2019"

  1. Congratulations sister!!!,this has really inspired me,work hard in every area in my life despite challenges,putting God first,together with hardwork💪.All the best to you,more success and blessings!!

  2. Sounds great awwe

Leave a Message

Your email address will not be published.

© Maktaba. All rights reserved.