ONE ON ONE:JINSI NILIVYOFAULU MITIHANI KUPITIA MAKTABA

This is a Trial Version of Social Share & Locker Pro plugin. Please add your purchase code into Licence section to enable the Full Social Share & Locker Pro Version.
Kwa majina naitwa Micah Kalaita, ni mwenyeji wa Gairo Morogoro. Nilimaliza elimu yangu ya sekondari (kidato cha nne) mwaka 2011 katika shule moja ya kata lakini kwa bahati mbaya matokeo yangu hayakuwa mazuri! Nilifanikiwa kupata ‘D’ moja tuu kati ya masomo saba niliyofanya mtihani, hivyo nikawa na division 0. Nilikata tamaa ya kuendelea kusoma kutokana na matokeo hayo na baada ya hapo nilianza kujishughulisha na kazi zingine.
Nilikuja Dar es Salaam mwaka 2017 kwa lengo la kutafuta chuo cha ufundi ili angalau nipate ujuzi utakaonisaidia siku za usoni. Nilifanikiwa kuanza mafunzo chuo cha ufundi Veta kilichopo Chang’ombe na baada ya kuhitimu mwaka wa pili (level II) mnamo mwaka 2019 ndipo nilipoona kuna haja ya kujiendeleza na masomo kupitia fani niliyokuwa nimeichagua. Ikumbukwe kwamba kadri unavyozidi kusogeza hatua mbele kimasomo ndivyo unavyozidi kujirasimisha kwenye mfumo wa elimu, kwani nilipotaka kuendelea na mwaka wa tatu (level III) nilipaswa kuwa na cheti cha kidato cha nne! Hivyo kama ilivyo ndoto yangu ya kuendelea mbele, nililazimika kutafuta kwanza cheti hicho. Nilifanikiwa kupata kituo cha kusomea cha GOOD HOPE CENTER kilichopo Ubungo nikiwa kama resitter mwaka 2021 nakuongeza juhudi kubwa kwa msaada wa walimu wa pale kituoni.
Kama ilivyo kawaida katika maandalizi ya mitihani mwanafunzi anahitaji kupata ‘past papers’ nyingi zaidi na kutoka sehemu tofauti tofauti ili aweze kujiimarisha kukabiliana vyema na mitihani yake ya mwisho! Na hicho ndicho kitu pekee nilichokuwa nakihitaji kwa wakati huo, nilijaribu kutafuta ‘materials’ kama vile ‘past papers’ kutoka sehemu mbalimbali ili kukidhi mahitaji yangu. Hatahivyo mwanzoni nilipata changamoto ya kutopata ‘full package’ kuanzia notes mpaka past papers za kila shule ili niweze kujiimarisha zaidi.
Mwanzoni mwa April 2021 katika harakati za kutafuta App za kujisomea kwenye simu yangu nilibahatika kukutana na App iitwayo MAKTABA ambayo kwa kiasi kikubwa ilikuja kujibu changamoto yangu kwani ilikuwa na ‘full package’ yani notes zote za ‘O level’, past papers za mikoa yote Tanzania pamoja na marking scheme zake tena kwa gharama nafuu kabisa ambayo mtu yeyote anaimudu! Nilijitahidi sana kuifanya hiyo mitihani kwa kushirikiana na walimu wangu pale kituoni, kusema kweli ile mitihani ilinijenga vizuri sana katika kujiandaa na mitihani yangu ya Necta kwani baada ya kumaliza mitihani salama November 2021 katika kituo cha kufanyia mitihani  cha Temboni Secondary school center chenye namba P.1363 hatimaye nilipata matokeo mazuri sana kwa upande wangu nikiwa na division II ya 20!
Ushauri wangu kwa vijana wote iwe QT ama RESITTERS nawaasa kuwa; ili kupata matokeo mazuri ni lazima watafute sehemu nzuri za kusomea ikiwemo kituo cha kusomea kama GOOD HOPE iliyopo Ubungo na vyanzo mbalimbali vitoavyo huduma za kielimu kama ilivyo App ya MAKTABA ambayo wanaweza kuipakua playstore katika simu zao HAKIKA HAWATAJUTIA kwani hizo ndizo sehemu pekee zilizonipatia division II, ukizingatia nilikaa kwa zaidi ya miaka 10 baada ya kumaliza kidato cha nne 2011! Hivyo kujiandaa kwa mwaka mmoja tuu na kupata matokeo mazuri kiasi hiki sio tu juhudi zangu bali pia ni msaada mkubwa nilioupata MAKTABA pamoja na GOOD HOPE.
Namshukuru sana Mungu kwa kufanikisha hitaji langu, sasa malengo yangu ni kuendelea na hatua za  mbele katika masomo yangu. 
Ahsanteni!

TUFWATILIE NA UPATE UPDATES MBALIMBALI KWA KUJOIN GROUP LETU LA WHATSAPP KWA KUFWATA HII LINK——->https://chat.whatsapp.com/BOVxXiclOtJJbJgqIjcZx2
Primary School: NIL
Primary School Year: 1900
Ordinary School: NIL
Ordinary School Year: 2010
Ordinary School Division: 2
High School: NIL
High School Year: 2021
High School Division: NIL
University Name: NIL
University Year: 2025
University GPA: NIL
University Course: NIL
Current Job: NIL
Current Company: NIL
Associate Gender: Male
Associate Advice on Studies: NIL
Associate Advice on Career: NIL

Related Articles

HOW TO TRAIN YOUR BRAIN TO FOCUS COMPLETELY ON STUDIES AND SUCCESS
WOMEN IN ENGINEERING
Wanafunzi 10 Bora Matokeo Darasa la Saba 2021
TECH INSIGHT WITH ELIAS RANGE
Some think these are most profitable digital products to sell online
NECTA Yatangaza Matokeo Darasa la Saba, Tazama Hapa
JIFUNZE NAMNA YA KUFANIKIWA KIMASOMO KUTOKA KWA ROSALIA! MWANAFUNZI WA NNE KITAIFA 2019
SIMULIZI YA MAFANIKIO YA HOPE – MWANAFUNZI BORA KITAIFA 2018
ONE ON ONE:JINSI NILIVYOFAULU MITIHANI KUPITIA MAKTABA

Recently Viewed

More articles will be added latter

0 responses on "ONE ON ONE:JINSI NILIVYOFAULU MITIHANI KUPITIA MAKTABA"

Leave a Message

Your email address will not be published.

© Maktaba. All rights reserved.