This is a Trial Version of Social Share & Locker Pro plugin. Please add your purchase code into Licence section to enable the Full Social Share & Locker Pro Version.
SIMULIZI YA MAFANIKIO YA MWANAFUNZI BORA KITAIFA 2018
1.Tuelezee kwa kifupi Hope ni mtu wa aina gani?
Hope ni kijana mwenye maono na ndoto, mpambanaji na asiyechoka kufanya chochote kufikia malengo yake. Anapenda kusoma vitabu, kujadili stori za maisha na vijana wenzake,pia kutengeneza marafiki wapya. Anapenda kujichanganya na watu, japo itategemea sana ni watu wa aina gani. Bila kusahau kusaidia watu pale wanapohitaji msaada wake, kwani naamini tunakua kwa kusaidia watu wengine.
2.Wewe, ulikua mwanafunzi wa kwanza kitaifa 2018, Tuelezee unahisi nini hasa kilikufanya ufanikiwe.
Jambo la kwanza ni Kumuomba Mungu. Nilikuwa nasali kabla na baada ya kusoma, Nilikua nina kauli mbiu yangu ambayo ni “2018SaliZaidi”. Nilikua nasali sana nitimize ndoto zangu, pia kuwa na maono. Nakumbuka kuanzia kidato cha pili nlikuwa naona nipo miongoni mwa wanafunzi bora kitaifa. Hivyo kila siku nilikuwa napambana kutimiza ndoto zangu. Bila kusahau kuheshimu ratiba nliyokuwa nimejiwekea, kwani niliamini ndio itanifanya nitimize malengo yangu ya siku. Pia kutokukata tamaa pamoja na changamoto zote nilizokutana nazo, Nakumbuka nilivoanza kidato cha kwanza, safari haikuwa rahisi, lugha ya kiingereza ilikua changamoto kubwa sana kwangu kwani nimetoka shule iliyokuwa inatumia lugha ya kiswahili kama lugha ya kujifunzia. Lakini sikukata tamaa, Nilihakikisha nakabiliana na changamoto hii kwa kusoma Vitabu vingi vya kiingereza na grammar, pia nikatengeneza urafiki na wanafunzi wenzangu ambao wako vizuri kwenye lugha ya kiingereza na kuwasihi waongee na mimi kwa lugha ya Kiingereza tu tukiwa tunawasiliana. Baada ya kukabiliana na hio changamoto ya lugha, changamoto nyengine zilikua ni kutokuelewa topic, ambapo nilihakikisha naomba Wanafunzi wenzangu wa vidato vya juu kunifundisha pia kufanya mazoezi zaidi kuhusu hio topic ili kuhakikisha naielewa vizuri zaidi kwani Wanasema “Practice makes Perfect”!.
3.Watu husema shule za Serikali hazina walimu bora na hazifaulishi, Kwa maoni yako, nini suluhisho kwa hii changamoto?
Kiukweli shule za serikali zina changamoto zake, labda kutokana na idadi ya wanafunzi waliopo na uhaba wa vitendea kazi. Lakini pia, kuna faida kusoma shule za serikali, na serikali inapambana kutimiza malengo yake ya kufanya mahitaji muhimu kwa wanafunzi kama maabara, vitabu n.k yanapatikana kwa urahisi.
Nadhani ufaulu ungeongezeka kwa kiasi chake, lakini jambo la muhimu ni kuongeza idadi ya shule ili kupunguza msongamano wa wanafunzi ndani ya darasa moja, hii itasaidia uelewa wa masomo kuwa mkubwa, na hii itapelekea ufaulu kuongezeka, pia wazazi na zile familia masikini watakuwa na uwezo wa kusoma bila vikwazo, kwa kifupi ufaulu utaongeza kwa kiwango cha kuridhisha.
-
Kuna watu wanasema hakuna umuhimu wa kufaulu sana, Kwan maisha hayaikisi Elimu ya darasani hata kidogo? Nini mtazamo wako juu ya hili?
Ni ukweli usiopingika kuwa elimu hufungua akili za watu na kufanya waone mambo kwa mapana zaidi. Suala la elimu kutoakisi maisha ya mtaani bado lina ukakasi. Hii inategemea na mtu anatumia vipi elimu aliyopata. Nadhani kuwa tayari kuendelea kujifunza mambo mapya na kutumia ujuzi na maarifa aliyopata darasani, ni silaha mojawapo kushinda maisha. Sio lazima uajiriwe, uwezo wako wa kujifunza ujasiriamali na kujihusisha na wale uliosoma nao, unaweza kukufanya ufanikiwe katika maisha yako.
-
Baada ya kuwa wa kwanza kitaifa, Jamii inakuona una kipawa cha kuleta mabadiliko katika nyanja mbalimbali, Una mawazo gani juu ya hili?
0 responses on "SIMULIZI YA MAFANIKIO YA HOPE - MWANAFUNZI BORA KITAIFA 2018"