Njia 7 za kufanya taaluma yako ikunufaishe kimapato ktk uchumi wa sasa wa kidijitari

This is a Trial Version of Social Share & Locker Pro plugin. Please add your purchase code into Licence section to enable the Full Social Share & Locker Pro Version.

Watu wengi wamepata elimu mpaka chuo lakini level za taaluma zao zimekuwa haziendani na level za mapato yao! Mapato yao yamekuwa chini tofauti na vyeo vya taaluma zao! Unaweza kuta mtu anaitwa engineer, doctor, mkemia, mwalimu, architect, economy analyst… na vyeo vingine vingi, lakini kima cha vipato vyao wao wenyewe wanaona kabisa ni vidogo na haviendani na uzito wa vyeo vyao.

Tangu tulivyokuwa wadogo tunasoma, mawazo ya wengi yalikuwa ni kufanikiwa kiuchumi kutokana na taaluma uliyochagua kusomea; kama ni mhandisi basi hali yako ya kiuchumi inaendana na mchango wa taaluma yako kwa jamii yako; kama ni doctor nawe hali ya kiuchumi inakuwa kulingana na cheo chako cha udaktari; kama ni mchumi au mwanasheria au mwalimu au nesi au marketing au accontants… hivyohivyo hali yako ya kiuchumi inaendana na hadhi ya taaluma yako! Hamna aliye fikiria mapato duni!

Well, matarajio ya wengi hayajawa hivyo! Hakuna haja ya kulalamika bali kama msomi unatakiwa upate kufikiri na  kuweza kuwajibika ili taaluma yako ikunufaishe vyema hata katika hali ya uchumi; lakini pia wale wanaokuona nao watiwe moyo na mafanikio ya taaluma yako ili nao wasonge mbele.

Zipo njia kadhaa ambazo unaweza zifanya ziweze kuboost taaluma yako ili ikunufaishe kiuchumi! Kutokana na mwelekeo wa Dunia na nchi yetu katika hali ya uchumi, basi nitaelezea njia chache ambazo ni za KISASA na unazoweza zitumia kuweza kuboost hali yako ya kiuchumi katika ulimwengu huu wa kidijitari!

Uchumi wa kidijitari

Nasisitiza uchumi wa kidijitari maana ndiko tulipo kiuchumi na ndipo tunapoendelea kuelekea zaidi kwenye uchumi huu. Hii ina maana mtu, biashara au taasisi yeyote ile ambayo haijaweza vyema kujiunganisha na uchumi huu wa kidijitari basi utakuta inafeli kiuchumi. Waweza angalia jinsi TIGOPESA, MPESA, MAXMALIPO, SELCOM… zilivyopata nguvu zaidi katika kufanikisha malipo ya watu katika sekta mbalimbali. Watu sasa hawaendi benki kuweka au kutoa pesa, bali moja kwa moja kwa kutumia simu zao wananunua umeme, lipia ving’amuzi, lipa ada, lipia faini za polisi, lipa kodi… moja kwa moja kwa kutumia simu zao zenye mitandao. Na tunapoelekea mbeleni zaidi na zaidi ndivyo uchumi wa kidijitari unavyozidi kushikilia sekta ya uchumi.

 • Jaribu kuangalia namna UBER inavyovuta watu kujiajiri kupitia simu zao! Watu wengi sasa wameacha ajira zao za zamani na kujiunga na UBER kupitia simu zao na wanasafirisha wateja kwa urahisi na kujijengea kipato zaidi! Yule dereva ambaye hayupo katika mtandao anakosa wateja maana wateja nao wanataka UBER kwasababu ya unafuu, urahisi na kuaminika!
 • Waweza angalia namna Facebook, Instagram, WhatsApp, Jamiiforums na mitandao mingine jinsi inavyobadili direction ya hali uchumi jamii! Sasa watu wanafanya vikao vya harusi moja kwa moja kupitia WhatsApp groups (hii ina maanisha kuwa hoteli zilizokuwa zinatoa huduma za sehemu za vikao vya harusi sasa zinapungua wateja).
 • Watu sasa wanatangaza bidhaa zao katika mitandao ya Kijamii; Hawa watu ni wengi sana na hawana hata duka au fremu aliyopangisha; moja kwa moja yupo nyumbani kwake anauza bidhaa kibao na kujenga kipato chake; gharama yake yeye ni bando tu la Tsh. 500/= ila yule aliyepanga fremu barabarani kwa Tshs. 200,000/= na ada kibao anatumia nguvu zaidi!
 • Waweza tazama pia namna ambavyo watu wanapata masomo mtandaoni hadi level za vyeti vya degree kabisa ambavyo vinatambulika. Wengine wamefungua magroup ya whatsApp na ili kujiunga unawalipa ili uweze kupata mafunzo yao ambayo wanafundisha. Wapo wengine ambao wanauza miziki, video, vitabu mtandaoni! Wapo wengine ambao wanauza ramani za nyumba, specifications za kitaalamu, wanafanya matangazo mtandaoni, wanafanya huduma za design za logo na card moja kwa moja mtandaoni. Hawa wote wanazidi nufaika na ufanisi wa uchumi wa kidijitari.

Kujiajiri Mtandaoni

Yapo mambo mengi ambayo tunaweza zungumzia kuhusu uchumi wa kidijitari na tunapoelekea! Lakini leo tuzungumzie namna ambavyo unaweza ufanya utaalamu wako ukunufaishe katika uchumi huu wa kidijitari kupitia mtandao wa Maktaba.ac.tz popote ulipo Tanzania au nje ya nchi! Haihitaji uwe na mtaji wa ma milioni au laki kadhaa, bali kinachohitajika ni NGUVU YA AKILI YAKO, YOUR MENTAL ASSETS ambayo obvious unayo na kwa miaka mingi umekuwa ukiinoa shuleni mpaka ngazi za vyuo. Unachopaswa ni kujiamini na kuchukua hatua.

Kupitia mtandao wa Maktaba.ac.tz mtu yeyote unaweza jenga kipato chako kwa kufundisha na kuuza bidhaa za kidijitari (downloadable softcopy) ili uweze kulipwa na wateja wako. Hivyo waweza uza downloadable softcopy katika mfumo wowote wa documents, ebooks, files, audio, video, templates, plugins, software, passwords, access keys, special spread sheets na aina yeyote ile ya softcopy. Mteja wako anakulipa kwanza moja kwa moja mtandaoni ndio kisha anaruhusiwa kufanya download ya softcopy zako. Malipo yanafanyika moja kwa moja mtandaoni kwa njia ya Mpesa, Tigopesa, Cards au eWallet kama Paypal. Mteja anaweza lipia akiwa popote pale Tanzania au nchi yeyote Dunia nzima. Malipo yanafanyika ndani ya dakika chache tu, hivyo kazi yako wewe ni kuandaa kazi iliyo na ubora.

Njia kunufaika kimapato ktk uchumi huu wa kidijitari kupitia taaluma yako

Njia ambazo kama msomi au mtaalamu unaweza zitumia kujenga kipato chako cha nguvu ili kuweza kunufaika kiuchumi na pia uweze kuendana na uchumi wa sasa wa kidijitari ni kama zifuatazo

 1. Uza docs, specifications, guidelines
  • Kwenye taaluma yeote ile kuna specifications, guidelines, indexes, formular na mambo mengine kibao ya mtindo huo. Mfano, kwenye engineering kuna starndards and materials rates; kwenye ualimu kuna miongozo ya masomo na guidlines; kwenye sheria kuna codes na vingine; kwenye kila taaluma kuna specifications mbalimbali ambazo zinabadilika kila muda. Mimi kama msomi ninaweza amua nikawa nafanya biashara ya kuzitafuta, kuziandaa vyema na kuziweka katika mfumo wa PDFs au DOCS na kisha nikawauzia wenzangu ili wao wasitumia nguvu kubwa sana kufanya kazi zao. Kama mimi ni mtu wa marketing ninaweza andaa marketing specifications za kitu fulani au bidhaa aina fulani au eneo fulani au kwa kampuni yetu na kisha nikaanza kuwauzia PDFs na kisha nijenge kipato changu.
  • Unachotakiwa ni kujiunga katika mtandao wa Maktaba na kisha ufungue digital shop yako na uanze kuuza mara moja kwa ufanisi na urahisi.
  • Je, ni specifications au guidelines gani ambazo kwenye fani yenu mmekuwa mnazitumia? Waweza orodhesha aina 20 ya specifications ambazo unaweza anza kuwauzia wataalamu wenzako na kisha ukachagua kadhaa za kuanza kuziuza! Kumbuka kuwa unapaswa uandae vyema na uendelee kuziboresha kila mara ili wawe wananunua kila toleo jipya utakalokuwa unalitoa.
 2. Uza magazines na ebooks
  • Watu wanahitaji kusoma na kuongeza maarifa. Kwa ufupi watu wanahitaji taarifa ambazo zitaweza kuwasaidia kutatua matatizo yao na kuyafanya maisha yao yawe bora zaidi. Kama ni mtu wa saikolojia basi wapo watu wengi ambao wanahitaji vitabu vyako ili waweze kusoma na kuboresha hali zao za akili! Kama ni mwalimu basi wapo wanafunzi wengi ambao wanahitaji vitabu vya topiki fulani ili waweze kuelewa vyema na kufaulu; wanafunzi pia wanahitaji vitabu vya maswali na majibu au solved examinations ili kujinoa kimitihani.
  • Waweza anza kuandaa majarida na magazeti yako kuhusu sekta, fani yako au topiki fulani ambazo umezichagua ili watu wapate taarifa na kisha waelimike na kusaidika. Andaa katika mfumo mzuri na jiwekee ratiba ya kuchapisha kwa mfumo wa matoleo kila baada ya muda fulani. Andaa katika mfumo wa PDFs na kuwauzia watu wako kwa kufanya downloads.
 3. Uza trainings materials
  • Training materials! Kwa kila fani ya taaluma kuna aina ya mitihani lazima uifanye ili uweze kupata cheti au muhuri au leseni! Unaonaje wewe uwe mmoja ya wataalmu ambao utakuwa unaandaa training materils na kuwauzia watu au wanafunzi wenzako ili kuwarahisishia maandalizi ya mitihani na wafanikiwe na kupata maksi za juu zaidi? Kama utaweza msaidia mtu ajiandae kwa siku 3 badala ya 7 na apate marks 90% badala ya 50% basi uwe na uhakika wapo watu wengi ambao watakuwa tayari kuweza kukulipa ili wapate training materials zako.
  • Unapaswa uweze kuandaa training matetils ambazo zipo straight to the solutions. Lakini kama ni za kuelimisha basi ziwe zile ambazo zinamfanya mtu aelewe kwa urahisi na undani zaidi. Kuwa mbunifu katika kuandaa training materials zako ili uweze kuuza kwa wingi zaidi!
  • Fikiria mfano,Wewe ni mtu wa accounting, na unaanda training materials kuwasaidia wanafunzi kufanya mitihani ya bodi:
   • Labda umeandaa booklets na kwa moja unauza kwa Tshs. 10,000/=
   • Idadi ya wanafunzi wanaofanya mitihani hiyo wapo 5,000 na wewe ukafanikiwa kuwauzia wnafunzi 1,000 tu ndani ya miezi 2
   • Mapato yako ya mauzo ni Tshs. 10,000 x 1,000 people = Tshs. 10,000,000/=
   • Kwahiyo mauzo yako ndani ya siku 60 ni Tshs. 10,000,000/= na ukumbuke hii sio Biko au Kubet bali ni JUHUDI ZENYE UHAKIKA, THE POWER OF MENTAL ASSETS!
   • Pia waweza uza past-trainings materils zako ambazo ulizitumia wewe kujiandaa pindi unasoma ili kumaximise zaidi fursa.
  • Bofya link hapa kujiunga na kuanza kuuza trainings materials kwa sekta mbalimbali ambazo umezichagua
 4. Uza reports and researches
  • Usifungwe na maneno research na reports na ukaona yanahitaji mtu kama profesa au phd holder ndiyo ayazoee. Kumbuka research ni utafiti tuu, yaani kama inavyosomeka kiswahili ni UTAFITI. Au Reports ni just ripoti yaani utupe mrejesho wa ulichoona. Kwa hiyo waweza anza kuandaa researches na ripoti za mambo kadhaa katika fani yako na kisha uanze kuziuza kwa wahusika mbalimbali ikiwemo serikali nao wafanye download katika duka lako mtandaoni!
  • Fikiri mimi ni mtu wa masoko ya kilimo, naweza andaa ripoti ya masoko ya bidhaa za kilimo ambazo kwa sasa zinauzika sana katika jiji la Dar es Salaam na kisha nikawauzia kwa kiasi cha Tshs. 5,000/= wakulima na wafanyabiashara jumla ya 500 hivi kila mwezi! Hiyo ikanijengea kiasi cha Tshs. 2,250,000/= kila mwezi.
  • Au nikawa mchambuzi wa uchumi na kuandaa ripoti zangu na kuziuza katika mfumo wa PDFs ili wasomaji wangu waweze kuzisoma. Kama nikiandaa ripoti ya uchambuzi wa uchumi na kuuza kwa Tshs. 200,000/= kwa watu na taasisi mbalimbali jumla zaidi ya 100… ipo safi! Hiyo ni kama Tshs. 20,000,000/=. Kuwa mbunifu kuifanya taaluma yako ikunufaishe kiuchumi na uweze kupata moyo zaidi wa kuifanya kazi yako kwa furaha na esteem zaidi!
 5. Uza consultations kwa njia ya checklists, self-assessments…
  • Utaalamu siku zote ni kutatua matatizo special ambayo jamii inayakuta. Kama ni fundi seremala basi unatatua matatizo ya kukaa kwa namna ya kuutumia mti kutengeneza sofa nzuri. Kama ni mwanasheria basi kuwasaidia watu katika kuichambua sheria na kuielewa ili wapate haki zao na kulinda haki za wengine.
  • Je, katika miwani ya fani yako unaona ni matatizo gani ambayo watu wengi Tanzania, Kenya wanapitia? Je, unayo solution ambayo inaweza wasaidia watu kuweza kutatua matatizo yao? Kwanini ubaki na solution wakati watu wanasumbuka na matatizo waliyonayo?
  • Unachotakiwa na kuandaa pre-designed checklists na guidelines ambazo msomaji ataweza zifuata ili kuweza kutatua matatizo yake.
   • Mfano waweza angalia matatizo ya nidhamu ya pesa, Jinsi ya kuhudumia bustani ya mbogamboga kisasa zaidi, namna ya kutengeneza mabwawa ya samaki kutumia mifuko ya plastiki…
   • Yapo matatizo mbalimbali ambayo waweza wasaidia watu kutatua kwa njia ya consultation utakazokuwa unawauzia wao. Kuwa makini kuhakikisha kuwa hauvunji sheria za nchi na fani yako.
  • Waweza andaa audios clips, video clips, PDFs, booklets za consultations za aina mbalimbali ili nao waweze fanya downloads mtandaoni baada ya kukamilisha malipo, hii itawasaidia kuweza kuboresha maisha.
 6. Uza pre-designed na pre-configured systems na templates
  • Waweza andaa pre-designed templates au systems na kuwauzia watu wako ili waweze kurahisisha kazi  zao na kufanya kwa ufanisi zaidi.
   • Waweza andaa ramani za majengo na ufundi, furniture, mashine na kisha kuwauzia wahusika ili nao waweza kufanya kazi zao kwa urahisi zaidi!
   • waweza andaa business plans za biashara kadhaa na miradi mikubwa kwa midogo na kisha kuwauzia watu wengi mtandaoni nao waweze kufanya biashara zao kwa ufanisi zaidi!
   • Waweza angalia fani yako huwa ina aina gani ya materiials ambayo kila mara huwa yanahitajika kuandaliwa – waweza yaandaa hayo yakiwa katika hali nzuri zaidi ya kutumia mara moja ili wapate ufanisi wa kuzitumia.
  • Kama ni mtaalamu wa kuandaa spreadsheets (ie. Microsoft excels) basi waweza andaa sheets ambazo mtumiaji kazi yake ni kuingiza data tuu mara moja then zenyewe zitoe majibu na kuchora chati fulani.
   • Wapo ambao wanatumia spreadseets kuandaa ripoti za maofisi, kufanya designing ya majengo na madaraja, kufanya mahesabu ya kibiashara, kuandaa bills of quantities, kufanya complex mathematics ya kitu fulani…
   • hivyo nawe waweza andaa spreadsheets kisha ukawauzia watu wako kwa gharama fulani ili kuwapa ufanisi wa kazi zao lakini na wewe ujenge kipato chako kwa nguvu; unachofanya wewe ni kuziandaa na kuzi-upload katika duka lako mtandaoni Maktaba na kisha kuwatangazia ili wafanye downlaods kwa malipo.
  • Kama ni mtaalamu wa IT waweza andaa games na software kisha ukawauzia watu wako ili nao waweze rahisisha maisha kwa kutumia software zako. Waweza andaa Andoid apps na kisha ukaziuza katika mfumo wa files na pia ukaweka maelezo mazuri ya namna ya kuinstall na kuzitumia. The limit is your thinking.
 7. Uza Graphics, audio, docs, video clips kwa wateja walio ndani na nje ya nchi
  • Unaweza andaa softcopy za aina mbalimbali kwa wewe jinsi utakavyo fikiri na ukaanza kuziuza kwa wateja wako mbalimbali walio nje na ndani ya nchi. Cha msingi ni kuhakikisha unaandaa vyema katika hali ya ubora, unatoa maelekezo mazuri ya namna ya kutumia, unafanya matangazo ya kutosha kuwavuta wateja wako na pia unatoa huduma nzuri kwa wateja wako kwa kuwajibu maswali na kusikiliza maoni na comments zao katika digital shop yako.

Hizo ni baadhi ya njia ambazo mtaalamu unaweza zifanya ili kuweza kuboresha hali yako ya uchumi katika uchumi huu wa kidijitari huku ukizidi kufurahia fani yako. Zipo njia nyingi za mtandaoni ambazo zinatumika kujenga kipato zaidi, bali kwa mtu uliye Tanzania na Afrika Mashariki hizi zinakupa urahisi na uhalisia kuzifanya na zikakujengea kipato chako kupitia mtandao wa Maktaba na ukapata mapato yako bila limitations za kimalipo.

Hamna mafanikio ya mteremko, bali ili ufanikiwe katika njia hizo hapo juu unahitaji uwe na utayari, passion, uandae vitu vilivyo bora na pia ujitoe kutangaza bidhaa kwa wateja wengi zaidi ili kuwavuta waweze kununua katika duka lako.

Njia hizi za mtandaoni zina urahisi na unafuu zaidi wa kumudu biashara yako popote pale ulipo, ukiwa nyumbani, safarini, mwanafunzi shuleni unasoma au upo ofisini unaendelea na ajira yako. Biashara na bidhaa zako masaa 24 zipo hewani kununuliwa, wewe unachotakiwa ni kufanya matangazo sana, kuzidi kuziboresha na huduma nzuri kwa wateja wako.

Dhamiria kuwa na mauzo ya maelfu ndani ya kila mwezi ili ujenge kipato kinachokutoa kimaisha kwa nguvu, kumbuka wewe ni mtaalamu umesota shule unapiga kitabu zaidi ya miaka 15. Yes inawezekana kuwa na mauzo ya elfu au kumi elfu; kumbuka Tanzania tuu tupo around watu 55,000,000 na watumiaji wa mtandao ni zaidi ya watu 23,000,000! Kwanini wewe ushindwe kuuza ONE ebook kwa watu zaidi ya 10,000? Bado hujangalia wateja walio Kenya, Uganda, Africa na Dunia nzima! Inawezekana!

Haina haja ya kubaki unaumia au kulalamika kuhusiana na hali ya uchumi wako, jambo la msingi ni kuwajibika na kuchukua hatua. Bofya link hapa ili kufahamu zaidi kuhusu mtandao wa Maktaba na kujiunga uanze kunufaika ktk uchumi wa sasa wa kidijitari.

4 responses on "Njia 7 za kufanya taaluma yako ikunufaishe kimapato ktk uchumi wa sasa wa kidijitari"

 1. Very Good and wise suggestion from you.

 2. There is visibly a bundle to realize about this. I suppose you made some good points in features also. Gerda Reinaldos Skolnik

 3. Some genuinely good information, Gladiolus I noticed this. Rivy Raimundo Graner

 4. Hello. This article was really fascinating, particularly because I was browsing for thoughts on this topic last couple of days. Sam Maximo Heather

Leave a Message

Your email address will not be published. Required fields are marked *

© Maktaba. All rights reserved.