• No products in the basket.

Career Inspiration

ONE ON ONE:JINSI NILIVYOFAULU MITIHANI KUPITIA MAKTABA

Kwa majina naitwa Micah Kalaita, ni mwenyeji wa Gairo Morogoro. Nilimaliza elimu yangu ya sekondari (kidato cha nne) mwaka 2011 katika shule moja ya kata lakini kwa bahati mbaya matokeo yangu hayakuwa mazuri! Nilifanikiwa kupata 'D' moja tuu kati ya masomo saba niliyofanya mtihani, hivyo nikawa na division 0. Nilikata tamaa ya kuendelea kusoma kutokana na matokeo hayo na baada ya hapo nilianza kujishughulisha na kazi zingine. Soma zaidi kujua Maktaba Ilinisaidiaje kufaulu!

Read More

Profile PhotoMaktaba Assistance27/01/2022

NECTA Yatangaza Matokeo Darasa la Saba, Tazama Hapa

NECTA Yatangaza Matokeo Darasa la Saba, Tazama Hapa BARAZA la Mitihani la Taifa Tanzania (NECTA), leo Jumamosi, Oktoba 30, 2021 limetangaza matokeo ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi 2021 (Matokeo ya Darasa la Saba mwaka 2021 ambapo watahiniwa 907,820 kati ya milioni 1.2 waliofanya mtihani huo wamefaulu sawa na asilimia 81.9. Akitangaza matokeo hayo Jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa NECTA, Dkt. Charles Msonde, amesema kuwa mkoa wa Dar es Salaam umefanya vizuri zaidi katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba kwa mwaka 2021, ikifuatiwa na Iringa na Mbeya. Msonde amemtaja mtahiniwa Eluleki Evaristo Haule kuwa ndiye mwanafunzi aliyepata alama nyingi zaidi kuliko wenzake. Kutazama Matokeo Darasa la Saba 2021 <>Read More

Profile PhotoDada Maktaba31/10/2021

Wanafunzi 10 Bora Matokeo Darasa la Saba 2021

Wanafunzi 10 Bora Matokeo Darasa la Saba 2021 Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) leo Jumamosi Oktoba 30, 2021 limetangaza matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba mwaka 2021 ambapo mwanafunzi aliyehitimu shule ya msingi St Anne Marie iliyopo mkoani Dar es Salaam, Eluleki Evaristo Haule limemtangaza ndiye aliyeibuka kinara katika matokeo ya mtihani ya Darasa la Saba 2021. Akitangaza matokeo hayo Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amesema watahiniwa bora kitaifa ni wale ambao wamepata alama nyingi zaidi kuliko wenzao kwenye masomo sita waliyotahiniwa. Amemtaja aliyeshika nafasi ya pili kuwa ni Happy Joseph Deus kutoka shule ya msingi Twibhoki ya Mkoa wa Mara na nafasi ya tatu ikienda kwa John Chacha Charles kutoka Twibhoki. Aliyeshika nafasi ya nne ni Joshua Mahende Jacob kutoka shule ya msingi Twibhoki iliyopo Mara pia, Eva Sebastian Chengula kutoka shule ya msingi Fountain of Joy ya Dar es Salaam ameshika nafasi ya tano, Joctan Samwel Matara kutoka Twibhoki ameshika nafasi ya sita. Barnaba Jumanne Magoto kutoka shule ya msingi Twibhoki ipo Mara ameshika nafasi ya saba, Rahma Ombi Juma kutoka shule ya Mtuki Highland iliyopo Dar es Salaam ameshika nafasi ya nane na nafasi ya tisa ni Juliana John Shimbala kutoka St Joseph’s nafasi ya kumi ameishika Jackline Manfredy kutoka shule ya Masaka iliyopo Dar es Salaam.Read More

Profile PhotoDada Maktaba31/10/2021

WOMEN IN ENGINEERING

Ellen Henrietta Swallow Richards was the first woman admitted to the Massachusetts Institute of Technology (MIT), graduated in 1873, and later became its first woman instructor. She was an industrial and environmental chemist and a pioneer in sanitary engineering and home economics.Mar 8, 2019. This article will help you on how to become the best and a great engineer that will create a better future for it's community.

Read More

Profile Photosako sicho10/10/2019

TECH INSIGHT WITH ELIAS RANGE

A general technology career insight to help aspiring students to pursue a career in the IT industry

Read More

Profile Photoelias range02/10/2019
© Maktaba. All rights reserved.